Kijana
Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa amebebwa
na shangazi yake Stella Mbuligwe mara baada ya kutoka kufanyiwa usafi
wa mwili kutokana na wazazi wake kutoweza kutoa ushirikiano kwa kijana
huyo..
Kijana
Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Ilemi jijini Mbeya ambaye
anatatizo la akili na ulemavu wa viungo akipelekwa ndani na shangazi
yake ,Stella Mbuligwe mara baada yaa kufanyiwa usafi na kupatiwa chakula
Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Kata ya Ilemi jijini Mbeya mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili akiwa amelala ndani ,kwa zaidi ya miaka 11 sasa kwa kile kinacho elezwa kuwa ni kufichwa ndani na wazazi wake ili kuondoa aibu ya familia . BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Mahali
anapo lala kijana Emanuel Fedrick (20)Mkazi wa Mwambeja Kata ya Ilemi
jijini kwa zaidi ya Miaka 11 sasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuficha
aibu ya familia.
******************
|
Na
EmanuelMadafa,Mbeya
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na
akili, amegundulika kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake
katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi Jijini hapa.
Kijana
huyo, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amejulikana kwa jina la Fredrick Emmanuel
ametajwa kuwa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje hali
iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wake .
Mmoja wa
majirani ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa Kijana huyo licha ya
kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo vya mikono na miguu,pia amezaliwa akiwa na
utindio wa ubongo hali inayomfanya kushindwa kuongea.
Amesema
wazazi wa mtoto huyo wamekuwa wakimfungia ndani ambapo hata wao hawakuluhusiwa
kuingia ndani ya nyumba hali iliyowafanya washituke na kutoa taarifa ili
kumuokoa kijana huyo.
Akizungumzia
tukio hilo , Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary Jama, amesema taarifa za
Ferdrick kuishi ndani ya nyumba hiyo walikuwa nazo lakini hawakuwahi
kupata taarifa za kwamba kijana huyo hatolewi nje.
“Sisi
tunafahamu ndani ya nyumba ya Emmanuel kuna mtoto ambaye ni mlemavu lakini
hatukuweza kufahamu mazingira anayoishi kijana huyu, nimeshuhudia kweli huu ni
unyanyasaji wa kijinsia, licha ya kutotolewa nje lakini kijana huyu anaonekana
amekosa chakula,”alisema.
Akizungumza
huku akionesha kutojali , Baba wa kijana huyo Emmanuel John , anasema
mwanae Fedrick, alizaliwa mwaka 2007 ukiwa ni uzao wake wa kwanza katika
familia hiyo na akufuatiwa na wenzake watatu ambao wote mungu amewajalia na
kuzaliwa wakiwa wazima.
Kufuatia
tukio hilo baadhi ya majirani wameomba mamlaka husika kuingila kati ili
kumsaidia kijana huyo kwani maisha yake yapo hatarini kutokana na wazazi
kutoonesha kujali .
Mwisho
Imeandaliwa
na Mtandao wa kijamii wa JamiiMojablog-Mbeya na Mtandao wa
Fahari News
No comments:
Post a Comment