Mfalme
wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per
Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki,
huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA
inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water. Anaandika Sultani Kipingo.
Twenty
Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music
Awards (KTMA) kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili
mfululizo za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi
vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18,
2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.
"Nimerudi
kuwachinja tena" anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi
katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini
Dar es salaam. "Nimerudi kurudisha sauti ya gharama kwa jamii. Sauti
inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua
kila mtu, " anaogeza.
Tayari Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer Mann Water.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Wakili
msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo
la kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa
Combination Sounds, Rowel Moses.
"Namkubali
sana Twenye Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa
kurekodi maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri
hapohapo", anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na wasanii nyota
kibao wakiwemo Lady Jay Dee, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella,
MB Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.
Twenty
Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa "Manemane"
uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo
saba kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati
zilikuwa ni "Tamaa Mbaya" na "Ya nini Malumbano" na "Maisha ya Bongo"
Mbali
na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu
ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada
ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za
kilimo. "Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu
ili kuwachinja tena" alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana,
Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi zake huku akishuhudiwa na Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto), Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment