Msimamizi Mkuu wa Radio TimesFM, Ron Fidanza akiwapa amasa vijana kusoma kwa bidii.Aliezea mchango wa
kipindi cha Campus Vibes kwa wanafunzi wa chuo: Times Fm imejikita kutoa
mchango wake kupitia kipindi cha Campus Vibes ili kujenga jukwaa la
mazungumzo kwa vijana na wanafunzi wa elimu ya juu,” alisema.
“Pia Times Fm imeanzisha program maalum ili kuwawezesha wasomi wa habari vyuo vikuu kufanya mazoezi kwa vitendo.”
Mkurugenzi
wa kampuni ya Maznat Bridal, Maza Sinare akiongea na katika mjadala
maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini,
ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya
kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi
Ijumaa saa 3 kamili usiku.
Mhadhiri
wa Lugha wa Chuo cha Ualimu DUCE, Mhe. Ruben Ndimbo akiwaasa vijana
kuacha kulalamika wajitume ili waweze kujikwamua kimaisha.
Mhariri Mkuu wa Times Fm, Zorha Malisa akiwashukuru wanafunzi kwa kuja.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde
Jumamosi hii amekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la kujadili changamoto
za ajira nchini lililoandaliwa na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM
na kuwahusisha wanachuo wa vyuo vya elimu ya juu mbalimbali nchini.
Akiongea
kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Protea jijini Dar
es Salaam, mheshimiwa Mavunde aliwaasa vijana kuacha kulalamikia ajira
wakati uwezo wa kujiajiri wanao.
Mhe.
Mavunde alisema kwa sasa mambo yamebadilika sana hivyo watoe fikira za
kumaliza chuo na kujiwekea fikra za kuajiliwa wakati wao wenyewe
wanaouwezo wa kutengeneza ajira kutokana na mambo watakayobuni kufanya.
Alisema
kuwa kwa sasa vijana wanayonafasi ya kubuni miradi na serikali
ikawasaidia kuiendeleza mbele kwa kuwapa mitaji ili waifanikishe.
"Vijana
acheni Kulalamikia ajira, zama za mababu zetu ajira zilikuwa za kutosha
ila kwa sasa kila mmoja akimaliza chuo akataka aje apate ajira
serikalini haiwezekani, hivyo nawaasa kujiwekea malengo ya kujiajiri
wenyewe ili muingine katika soko la ushindani," Mhe. Mavunde.
Pamoja na mambo mengine, alisisitiza umuhimu wa muda. “Muda ni kitu cha msingi na kukitunza sana,” alisema.
“Nilikuwa
na ndoto ya kuja kuitumikia jamii, nilikataa kazi nyingi za kuajiriwa
ili kuifuata ndoto yangu, nilikuwa naamini maisha yangu yapo kwenye
siasa, mpaka sasa niliitambua njia yangu na ndio njia niliyopitia,”
alisisitiza.
Kwa
upande wake MC Pilipili ambaye pia alikuwa mmoja wa wazungumzaji,
alisema kuzaliwa kwenye familia maskini hakumaanishi kuwa huwezi
kujinasua na kuwa na maisha unayotaka.
“Usikasirike
kuzaliwa katika familia ya kimasikini sio kosa lako, jukumu lako ni
kujiondoa katika umasikini,” alisema mchekeshaji huyo ambaye pia ni
mtangazaji wa kituo hicho cha redio.
“Mungu
kila mtu kampa kipaji angalia jambo gani linajitokeza sana katika
maisha yako, usifate mkumbo, niliamua kukifata kipaji changu katika
kuchekesha.”
BAADHI
ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar
es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus
Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto
ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm
radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya
Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.
Mkurugenzi msaidizi wa Tanzania Patriotist Network (TAPANET) akielezea changamoto zinazowakabiri vijana.
Mwanafunzi wa UDSM, Eze Bernard akimuuliza swali Naibu Waziri Mhe. Mavunde.
Mwanafunzi wa DIT, Neema Pambe akiuliza swali.
Wanafunzi wakipata ukodak na Maibu Waziri Mhe. Mavunde.
Nilipata
ukodak na Mhe. Mavunde na Mc Pilipili mara baada ya kumaliza kongamano.
Nikiripoti kutoka eneo la Tukio ni Mimi Cathbert Kajuna wa Kajunason
Blog (kwanza kulia).Picha/Habari na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment