July 26, 2016

MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA YAMTIA HATIANI MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANAHABARI MWANGOSI

 Ulinzi  wa  polisi  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya  Iringa  leo  kabla ya  mtuhumiwa wa mauwaji  kufikishwa
 Wananchi  wakiwa  foleni  kukaguliwa  kabla ya  kuingia  mahakamani leo
 Msafara  wa  gari  za  FFU  zilizomsindikiz askari  mwenzao aliyekutwa  na kosa  la  kuua bila  kukusudia jana.
 Askari  wa FFU  wakitoka  mbio  mahakamani  hapo
 Wananchi  na  wanahabari  wakitoka  mahakamani  hapo 

Wakili  kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za  binadamu ((THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo 
 Siku ambayo  mwanahabari  Daudi  Mwangosi  alipouwawa
 Askari  hao   wakimtoa mahakamani  hapo  leo  mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi
                               Marehemu  Mwangosi  enzi  za uhai  wake.
***********
Na  MatukiodaimaBlog Iringa
MAHAKAMA   kuu  Kanda  ya  Iringa   imemtia hatiani   kwa   kosa la  kuua bila  kukusudia  askari  Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa  G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa  kuuua  mwaahabari  Daudi  Mwangosi   mwaka 2012 katika  kijiji  cha  Nyololo  wilaya ya  Mufindi.

Huku   wakili  upande  wa jamhuri  katika  kesi  hiyo  Adolph Mwaganda akiiomba  mahakama   hiyo  kutoa   hukumu  ya  kifungo  cha maisha  jela  kwa askari  huyo ambae  hata   hivyo  alisema upande wa  jamhuri  hauna  taarifa  za  makosa yoyote  aliyopata  kuyafanya.

No comments:

Post a Comment