July 20, 2016

KAMPENI YA NUNUA,UZA,SHINDA NA KONYAGI YAZINDULIWA MKOANI MBEYA

Meneja masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe  akizungumza na wadau na wasambazaji (hawapo) wa vileo aina ya konyagi kwenye ukumbi wa Hotel ya Beaco Jijini Mbeya.
Baadhi ya wasambazaji kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini walishiriki uzinduzi wa Kampeni ya Nunua, Uza Shinda ya Konyagi Jijini Mbeya na kuuliza maswali.
Baadhi ya wasambazaji kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini walishiriki uzinduzi wa Kampeni ya Nunua, Uza Shinda ya Konyagi kwenye Hotel ya Beaco Jijini Mbeya
Baadhi ya wasambazaji kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini walishiriki uzinduzi wa Kampeni ya Nunua, Uza Shinda ya Konyagi kwenye Hotel ya Beaco Jijini Mbeya.
Wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
********
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake,  imezindua  kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake kanda ya Nyanda za juu  itakayodumu kwa muda wa wiki 12.

Kanda hiyo ya mauzo inajumuisha mikoa ya Mbeya,Iringa,na  mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Beaco  mjini Mbeya jana , Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe  alisema “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni  kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Katika kufanikisha suala hili wasambazaji wetu 2 watakaoibuka kila mmoja atajishindia lori jipya la usambazaji vinywaji aina ya Eicher lenye uzito wa tani 3”.

Pia alisema kuwa wasambazaji wa bidhaa za kampuni wataweza kujishindia zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha kampeni lengo kubwa ni kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuongeza mapato yao ikiwemo kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla.

Bwana  Kavishe alisema katika shindano hili  wasambazaji wa bidhaa za TDL wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa 10. “Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”

No comments:

Post a Comment