July 14, 2016

DC KASULU APOKEA MSAADA WA MADAWATI 100 KUTOKA OXFAM



Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Col. Martin Mkisi akipokea msaada wa maadawati 100 kutoka Taasisi ya Oxfam ambayo yalikabidhiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Jane Foster. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Kasulu leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col. Martin Mkisi akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Jane Foster kwa msaada wa madawati 100 aliyotoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Col. Martin Mkisi akiwa na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Kasulu, Fatina Laay (kulia) na katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Jane Foster.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col. Martin Mkisi akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Jane Foster kwa msaada wa madawati 100 aliyotoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col. Martin Mkisi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kupokea msaada wa madawati kutoka Oxfam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Jane Foster akifuatiwa na Mkurugenzi wa Hlamashauri ya Kasulu, Fatina Laay pamoja na watendaji wengine wa hlamashauri hiyo.
****************
HALMASHAURI ya Wila ya Kasulu Mkoani Kigoma leo imepokea msaada wa Madawati 100 kutoka Taaisi ya Oxfam, ikiwa nikatika jitihada za Taaisi hiyo kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kusomea kwa wananfunzi nchini.

Akipokea msaada huo kutoka kwa Mkurugenzi Mkkazi wa Oxfam, Jane Foster, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col. Martin Mkisi alisema Wilaya yake inashukuru kwa msaada huo kwani umekuja katrika kipindi ambacho bado kazi ya utengenezaji madawati inaendelea.

Col. Mkisi alisema kwa kuunganisha nguvu za wadau na serikali ndipo pekee ambapo kuna weza kumaliza changamoto hiyo ya madawati nchini na hususani katika halamashauri yake ya Kasulu.

Aidha Col. Mkisi ametoa wito kwa wadau wengine mbalimbali waliopo Wilayani Kasulu na nje ya Kasulu kuiga mfano huo wa Oxfam katika kuendeleza ustawi wa wananchi wa Kasulu katika Nyanja mbalimbali kamavile afya, Elimu, Maji na shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Wilaya ya Kasulu imesha tekeleza agizo la utengenezaji madawati lililotolewa na Rais John Magufuli kwa asilimia zaidi ya 75 na jitihada zinaendelea kumalizia idadi iliyobaki ili kuwawezesha watoto wote wa shule za msingi na sekondari kukaa katika madawati.

No comments:

Post a Comment