July 13, 2016

DC KAKONKO AGIZA WATENDAJI WILAYANI HUMO KUTHIBITI UHARIBIFU WA MAZINGIRA



 Col. Hosea Maloda Ndagala, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma.
*******
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Col. Hosea Ndagala amewataka wananchi Wilayani humo kutunza mazingira na kuacha tabia za kuchoma moto misutu.

Col. Ndagala aliyasema hayo Julai 12,2016 wakati wa wa kikao chake na watendaji wa Kata, Vijiji na Viongozi mbalimbali wa halmashauri wakati wa kikao cha maandalizi ya ujio wa Mbio za Mwenge utakaotimua mbio zake wilayani humo hivi karibuni.

“Tunatatizo la uharibufu wa mazingira katika maeneo yetu tunayo yasimamia, watu wamekuwa wakiharibu mazingira kwa kuchomo moto hovyo mapori na misitu yetu jambo ambalo linachangia sana uharibifu wa mazingira,”alisema Col. Ndagala.

Amewataka viongozi hao wa wananchi kuhakikisha wanawahimiza na kuwasimamia wananchi katika suala hilo la uhifadhi mazingira na kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wananchi juu ya athari za uchomaji moto mapori na kuachana na tabia hiyo ya uharibufu wa mazingira.

Uchomaji hivyo misitu umekithiri sana katika maeneo mengi ya Wilaya ya Kankonko Mkoani Kigoma na hufanywa na wananchi wakati wa kuandaa mashamba au katika shughuli za uwindaji.

Kuhusu mbio hizo za mwenge wa Uhuru amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge huo ambao unakuja Wilayanai humo kuhamasisha upendo na amani pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni kuizindua na kuweka mawe ya msingi.

No comments:

Post a Comment