June 07, 2016

PS3 YATOA MAFUNZO MKOANI MWANZA

Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Rasilimali wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)  Josephine Kimaro akitoa mafunzo kwa viongozi wa sekta ya Afya waliojitokeza kushiriki semina hiyo mkoani Mwanza.
***************
NA MWANDISHI WETU, Mwanza
SHIRIKA  la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) kupitia mradi wake wa  Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) limeendesha mafunzo kwa watumishi Mkoani Mwanza kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo wa PS3 jijini Mwanza

Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Rasilimali watu cha Mradi wa PS3, Josephine Kimaro alisema kuwa lengo kubwa la kuzindua mradi huo ni kuhakikisha wanaimarisha mifumo katika sekta ya Umma katika mifumo ya Utendaji, mifumo ya mawasiliano pamoja na mifumo ya fedha.

Semina hiyo itadumu jijini hapa kwa siku tano  huku washiriki wakiwa ni  kuwa wizara ya afya, Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi na Ofisi ya Rais Utumishi ikiwa na kufundishwa namna ya uandaaji mzima wa bajeti ya watumishi kwa Mkoa wa Mwanza.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. Leonard Subi ambaye alikuwa mgeni rasmi  katika semina hiyo alisema kuwa wameupokea mradi huo kwa furaha kubwa kwani wanaenda kupata elimu kuhusu mifumo mbalimbali lengo ikiwa ni kuhakikisha kuwa sekta ya Afya inaendeshwa ipasavyo.

  “ Tumejisikia fahari sana baada ya kupata mradi utakaosaida mkoa kuimarisha mifumo yake hivyo tutanufaika kwa mengi katika semina hii huku akiataka washiriki wote  kuwamakini kwa lengo la kuwa mabarozi mazuri,” alisema

Alisema serikali imishaanisha Mikoa ambayo ina hali mbaya zaidi ya upungufu wa watumishi wa sekta ya afya Mwanza ikiwa miongoni pamoja na Kigoma Shinyanga.

 Mgeni rasmi katika semina hiyo DR Leonard Subi akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo jijini Mwanza.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini.

No comments:

Post a Comment