June 13, 2016

NEWALA WAKARIBIA KUFIKIA LENGO LA UTENGENEZAJI MADAWATI

 Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara, Christopher Magala (wapili kushoto walioketi) akiwa na maafisa wa Wilaya wakikagua kazi ya utengenezaji madawati kwaajili ya shule za Msingi na Sekondari Wilayani humo jama
 Sehemu ya madawati hayo yakiwa karakana
KASI ya utengenezaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari kwa Halmashauri Nyingi nchini linazidi kushika kasi ambapo Wilaya ya Newala mkoani Mtwara imebakisha madawati 878.

Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala alisema kasi ya utengenezaji huo wa madawati inakwenda vizuri na wanataraji kukamilisha kazi hiyo kabla ya muda uliotolewa na Rais kumalizika. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 “Wilaya yangu inaendelea vyema na kazi utengenezaji wa madawati, meza na viti vya walimu kwaajili ya shule zetu za Msingi na sekondari na wakati wowote tutamaliza kazi hiyo ndani ya muda ambao ulitolewa kuwa tuwe tumekamilisha,”alisema Magala.

Magala alisema Mahitaji ya madawati katika Wilaya yake ni  23,178 na madawati yaliyopo hadi sasa ni 20,515 na upungufu ukiwa ni madawati 2,863.

Alisema tangu kutolewa kwa agizo la utengenezaji wa madawati na Rais John Magufuli tayari madawati 1,585 yamesha tengenezezwa na idadi iliyobaki ni madawati 878.

Aidha Magala alisema wadau mbalimbali wa maendeleo waliopo ndani na nje ya Newala waliahidi kuchangia kazi hiyo ya utengenezaji madawati na kuwataka kutekeleza ahadi zao hizo.

“Wapo wadau wa maendeleo walipo ndani na nje ya Newala ambao walituahidi kuchangia kazi hii ya utengenezaji wa madawiti, hivyo ningependa kuwakumbusha kupitia taarifa hii kuwa wakamilishe ahadi zo ili malengo kwaajili ya kusaidia watoto wetu yatimie,”alisema Magala.


Rais Dk John Maguli wakati anawaapisha wakuu wa Mikoa Mwezi Mcahi mwaka huu alitoa miezi mitatu kwa kila mkoa kuwa umekamilisha utengenezaji wa madawati kwaajili ya shule za msingi na Sekondari. 

No comments:

Post a Comment