June 22, 2016

MKUTANO WA WADAO WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa taarifa kuwa itakutana na  wadau wake wote siku ya  ALHAMISI  TAREHE 23 JUNI  21016, ili kupokea  na kujibu malalamiko, kero, hoja na maoni mbalimbali kuhusu Utendaji kazi wa Ofisi ikiwa ni maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016.

Mkutano huo utafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 9:00 Alasiri katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.

Wadau wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaombwa kuhudhuria katika Mkutano huo muhimu.

Imetolewa na:                                    

Gerson Mdemu

NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

No comments:

Post a Comment