June 12, 2016

MAFUNZO YA PS3 KWA WATALAAM WA AFYA MKOA WA MWANZA YAFUNGWA

Mkufunzi wa mafunzo hayo ya wiki moja kwa maofisa na wataalam wa Afya mkoani Mwanza wakiendelea na mada katika semnina hiyo ya uimarishaji wa Mifumo katika sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Washiruiki wa mafunzo ya wiki moja kwa maofisa na wataalam wa Afya mkoani Mwanza wakiendelea na mada katika semnina hiyo ya uimarishaji wa Mifumo katika sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Washiruiki wa mafunzo ya wiki moja kwa maofisa na wataalam wa Afya mkoani Mwanza wakiendelea na mada katika semnina hiyo ya uimarishaji wa Mifumo katika sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Baadhi ya washiriki wakiwa katika pozi la picha.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Picha ya maafisa afya wakiwa pamoja na na wakufunzi wa mkutano huo.
***********
SHIRIKA la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID)kupitia mradi wake wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (PS3) limekamilisha mafunzo maalumu kwa wataalam wa sekta za afya na maofisa rasilimali watu katika sekta ya afya jijini Mwanza.

Akizungumza jana jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo Mkufunzi mkuu wa semina hiyo Martine Mapunda kutoka wizara ya Afya amesema kuwa semina hiyo ililenga kutatua tatizo la upungufu wa wahudumu wa Afya, ikiwemo kuongeza ajira kwa wahudumu wa afya hivyo washiriki wa semina hiyo wakitilia maanani kile walichojifunza wataweka usawa watumishi katika vituo mbalimbali vya afya jijini hapa ili wananchi waweze kupata huduma za Afya kwa usawa” alisema

Aidha Mapunda alisema kuwa wamewawezesha washiriki katika semina hiyo kuhakikisha kuwa watumishi wa Afya waliopo wanatumika vizuri ipasavyo ili huduma za Afya kwa wananchi ziendele kupatikana kwani zipo baadhi ya sehemu kuna watumishi wa Afya wengi huku sehemu zingine kukiwa hakuna watumishi kabisa hivyo Semina hiyo ambayo imefanyika kwa siku tano itawasaidia wakuu wa idara za afya katika wilaya husika wanawapanga wale watumishi wa Afya ili kuwe na usawa katika utoaji huduma

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Elina Msangi amesema kuwa mafunzo waliyoyapata katika semina hiyo yatawasaidia sana jinsi ya kupanga watumishi katika vituo vya Afya ili wananchi wasiwe wanateseka kupata huduma hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuweka idadi sawa ya watumishi kulingana na idadi ya vituo vya Afya vilivyopo katika wilaya husika.

No comments:

Post a Comment