Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akizungumza baada ya kukagua madawati na kuagiza kua madawati yakabidhiwe katika shule kwa maandishi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezitaka halmashauri zote kuzikabidhi shule madawati yote ya likamilika kwa maandishi ili kuepuka udanganyifu na madawati hewa
Hayo ameyasema leo katika ziara yake ya kikazi halmashauri ya Busokelo wilaya ya Rungwe kukagua kazi ya utengenezaji wa madawati katka halmashauri.
Amewashukuru wananchi, wadau na viongozi wa ngazi zote katika halmashauri zote Mkoa wa mbeya kwa namna walivyohamasika kuchangia utengenezaji wa madawati na anaamini Mkoa wa Mbeya itatekelezwa agizo la kukamilisha madawati ifikapo tarehe 30 juni ila kwa ajili ya kujiwekea sawa Mkoa umejieleza malengo ya kukamilisha tarehe 20 Juni na kuna kila dalili zoezi hilo litakamilika kama ilivyopangwa.
Amewataka viongozi wa halmashauri na watendaji kuyakabidhi madawati yote yaliyokamika kwa maandishi ili kudhibiti taarifa za madawati hewa kuficha ukweli na baadaye ibainike bado kuna upungufu.
"Naomba mkabidhi kwa kurejea taarifa ya upungufu kwa kila shule na si vinginevyo," alisema Makalla.
No comments:
Post a Comment