June 02, 2016

HALMASHAURI ZA BUTIAMA NA RORYA KUTEKELEZA MRADI WA PS3 AWAMU YA KWANZA MKOA WA MARA

 
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Felix Lyaniva wakifuatilia mada katika mafunzoa ambapo Halmashauri za Wilaya zao za Butiama na Rorya mkoani Mara ndio zimechaguliwa kuwa za kwanza kuanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za umma(PS3) katika sekta za afya, elimu na kilimo.
***************

HALAMSAHAURI Za Wilaya ya Rorya na Butiama mkoani Mara zimechaguliwa kuwa za kuanza utekelezaji wa mradi Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maemdeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Tayari watendaji kutoka halamshauri husika wanapatiwa mafunzo ya siku moja leo na wiki ijayo madiwani wao nao watapatiwa mafunzo maalum ya namna ya kushiriki utekelezaji wa mradi huo. Mafunzo hayo ya wiki moja yatafanyika mjini Bunda. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 Awamu ya pili pitatekelezwa mkoani Mara  kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Novemba na Desemba mwaka huu na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Bunda, Wilayaya Bunda, na Wilaya ya Serengeti. Huku Halmashauri ya Mji wa Musoma, Halamshauri ya Wilaya ya Musoma, pamoja na Halmashauri ya Wilaya Tarime na Halmashauri Mji wa Tarime zenyewe zikitaraji kuanza mwezi Machi na Aprili 2017.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.

Mradi wa PS3 utatekelezwa katika miakoa 13 ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga ambapo Halmashauri 97 zitahusika na utekelezaji wa mradi huo. Ambapo hadi sasa Hlamashauri 20 zimeshapitishwa kuanza utekelezaji katika mikoa 10.

 Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa (kushoto) akijadiliana jambo na Meneja wa Mifumo ya Mawasiliano wa PS3 Giovanni Dipiazza
 Mwakilishi wa  Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula (kushoto) akizungmza na Meneja wa Fedha na Utawala wa PS3, Benard Kilembe.
Afisa miradi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) anaeshughulika na Sera na Ushauri, Christina Godfrey akinukuu baadhi ya dondoo za majadiliano ya kundi la Halmashauri ya Rorya.
 Uwasilishaji wa kazi za vikundi kutoka kila halmashauri ulifanbyika kwa kila hamashauri.
 Washiriki kutoka PS3 na wadau wengine wakifuatilia uwasilishaji huo.
 Viongozi wa Wilaya na Mkoa wakifuatilia kwa makini uwasilishaji huo. Kulia ni ni Kaimu RAS mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akifuatiwa na DC wa Rorya, Felix Lyaniva, DC wa Serengeti Ally Maftah na DC wa Butiama, Annarose Nyamubi
 Wakuu wa Wilaya kutoka kulia ni DC wa Rorya, Felix Lyaniva, DC wa Serengeti Ally Maftah na DC wa Butiama, Annarose Nyamubi wakifuatilia kwa makini uwasilishaji huo.
 washiriki wakifuatilia mada
 Eva Kinunda wa PS3 akiwajibika katika dawati lake la uratibu
 Washiriki wakisikiliza uwasilishaji wa majadiliano ya vikundi vya Halmashauri
 Wawakilishi kutoka Halmashauri wakiwasilisha taarifa zao 
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, Ally Maftah (kushoto) ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara katika mafunzo ya mradi wa uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya umma (PS3) katika sekta za afya, elimu na Kilimo akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Felix Lyaniva.
 Uwasilishaji ukiendelea...
 Maswali yaliulizwa na washiriki kupata ufafanuzi zaidi
 Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.

 Mmoja wa wakurugenzi akichangia mada.
Mshauri wa Mambo ya Utawala Bora katika mradi wa PS3 kutoka Taasisi ya Ushauri ya TMA, Dk Chinuno Magoti akitoa ufafanuzi.


Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce Muro akifafanua na kujibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa katika idara yake katika utekelezaji wa mradi huo.

No comments:

Post a Comment