May 24, 2016

MWANZA KUPOKEA TANI 500 ZA SUKARI KUTOKA KAGERA SUGER

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wa Mwanza unategemea kupokea Tani 500 za Sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H  Shah.

Hata hivyo mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei elekezi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa nipamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.

Mongella amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.

Mahitaji ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 ukweli kwamba itasaidia kupunguza uhaba wa sukari  unao ukabili  mkoa huu kwa sasa.

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema, tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA

24, Meil 2016

No comments:

Post a Comment