Afisa Rasilimali watu katika kiwanda cha TBL mkoani Mwanza, Dorah
Nyambalya akifanya tathimini ya kazi kwa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho
jana.
Dorah
Nyambalya akiendelea na kazi ya kufanya tathimini ya kazi kwa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho
jana.
Dorah
ambaye ni Afisa Rasilimali watu katika kiwanda cha TBL mkoani Mwanza, alifanya tathimini ya kazi kwa mfanyakzi mmoja mmoja.
Dorah ambaye ni Afisa Rasilimali watu katika kiwanda cha TBL mkoani Mwanza, alifanya tathimini ya kazi kwa mfanyakzi mmoja mmoja.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Mwanza wakiwa katika picha ya
pamoja baada ya zoezi la tahmini kiwandani hapo leo.
******************
KAMPUNI ya TBL Group kuanzia leo imeanza kuendesha zoezi la kutathmini
wafanyakazi wote katika viwanda vyake vyote vilivyopo katika mikoa ya Dar es
Salaam,Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro.
Lengo kubwa la kuendesha zoezi hilo limeelezwa kuwa ni kujua changamoto
wanazokabiliana nazo wafanyakazi katika majukumu yao ya kila siku ili
kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuleta ufanisi wenye tija katika kazi.
Katika kutekeleza zoezi hilo wafanyakazi walijaza fomu maaalumu zenye
maswali ya kiutendaji chini ya usimamizi wa watendaji wa idara ya Raslimali
watu ambao yalihusu utendaji wao,changamoto wanazokutana nazo pia walipata
fursa ya kutoa maoni yao ni jinsi gani ya kuboresha mazingira ya kazi na
kuwaendeleza wao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment