Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiongea na
baadhi ya wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika
kwenye viwanja vya TTCL Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wakati wa
madhimisho ya siku ya hedhi Salama mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiwagawia
kinywaji cha Grand Malt baadhi ya wazazi wa watoto wanaosoma katika
shule mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya TTCL Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi Salama
mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa
Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo wakati wa maadhimisho hayo.
***********
MENEJA Uhusiano wa nje wa kampuni ya TBL Group,Emma Oriyo, amesema kuwa
jukumu la kuwainua watoto wa kike nchini sio la serikali bali linamhusu kila
mtanzania ikiwemo makampuni,taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani iliyoadhimishwa
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ,alisema kuwa siku hiyo ni muhimu
kuadhimishwa kwa kuwa inatukumbusha watanzania kutofumbia matatizo yaliyopo kwenye
jamii yetu na kuangalia namna ya kuyashughulikia.
“Hapa Tanzania Changamoto za hedhi kwa watoto wa kike ni kubwa wengi
wakiwa wanakosa vifaa vya kuwaweka salama pia shule nyingi hazina miuondombinu
rafiki kwa wasichana kujiweka salama wanapokuwa kwenye hedhi,matokeo yake wengi
wanakuwa hawahudhuri masomo na kujikuta wamebaki nyuma ya wenzao wa
kiume”.Alisema.
Amesema TBL Group katika miradi yake ya afya ya kusaidia jamii imeanza
kuliangalia suala hili kwa undani ili kuweza kushirikiana na wadau wengine
kukabiliana nalo “Leo kampuni yetu ni moja ya wadhamini wa tukio hili la siku
ya hedhi ambalo lengo lake kubwa ni kuelimisha jamii umuhimu wa kuungana
kuondoa changamoto na hedhi na tutaendelea na jitihada hizi na kutekeleza
miradi mingine ya kusaidia kuboresha afya nchini”.Alisema.
Alisema watanzania wakiungana na serikali katika
kukabiliana na changamoto hizi hali itakuwa nzuri na watoto wa kike
kusoma katika mazingira mazuri na itapelekea wafanye vizuri kwenye masomo yao
sambamba na wenzao wa kiume.
Emma alisema kuwa hali ya kukosa vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi na
miundombinu isiyo rafiki mashuleni mbali na utoro mashuleni pia inawasabishia
watoto wa kike kutojiamini na wakikua bila kujiamini wanakuwa hawawezi
kutoa maamuzi sahihi.
“Wadau wote tukiungana katika suala hili tutaweza kutekeleza dira ya
maendeleo ya taifa ambayo kwa upande wa elimu ina kauli mbiu isemayo Elimu Bora
bila ubaguzi inawezekana.Timiza wajibu wako”
No comments:
Post a Comment