October 07, 2015

WASHIRIKI BSS WAJINOA TAYARI KWA FAINALI HAPO KESHO

Mshiriki wa BSS Nassib Fonabo (mwenye gitaa) akiwa na Anger Mary wakifanya mazoezi kwa pamoja.
Nassib Fonabo (mwenye gitaa) akiimba  wakifanya mazoezi kwa pamojaion
Mshiriki wa BSS Jackline Kayengi  akionyesha uwezo wake katika mazoezi ya mwisho mwisho.
Na Mwandishi Wet
IKIWA kesho ndio fainali za shindano la Bongo Star Search, BSS kwa mwaka huu washriki wa shindano hilo wameendelea kujinoa kikamilifu huku kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi.

Washiriki hao walikuwa wakifanya mazoezi yao ya mwisho jana ambapo walionekana wakifanya mazoezi hayo kwa bidii zaidi.

Kila mshiriki alionekana kujiamini zaidi huku kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi wa shindano hilo ambapo mshindi anaondoka na kitita cha Milioni 50 pamoja na nyongeza ya mkataba wa kusimamiwa kazi zake za sanaa  na hivyo kufanya kuwa na thamani ya Milioni 60.

Kila mmoja alipokuwa akihojiwa na wanahabari alionekana kuonesha kuwa na imani na ushindi huku wakionesha uwezo wao wa kuimba pamoja na kucheza

Washiriki wa mwaka huu ni Frida Amani, Kayumba Juma, Angel Kato, Nassib Fonabo, Jaqline Kakenzi and Kelvin Gerson.

Shindano hilo linafanyika katika Ukumbi wa King Solomoni Hall uliopo karibia na Eaters Point Namanga ambapo kiingilio ni Elfu 25, 50 na 100,000/=

Kutakuwa na burudani kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria ambae anawasili leo na pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Band, Peter Msechu, Kala Jeremiah, Navy Kenzo, Ben Pol pamoja na msanii huyo wa Nigeria.

Wadhamini wa shindano hilo kwa mwaka huu ni pamoja na Huaweii, Salama Condom, Coca Cola, Kiwi, Fast Jet, Jubilee Insurance, Radio Clouds na Regency Hotel.

Tiketi zinauzwa katika maeneo mbalimbali kama vile Roby One fashion Sinza na Kinondoni, American Nails Kinondoni, Engen Petrol Station, Cloud Fm, Eaters Points Namanga, Shear Illusion Mlimani City.

No comments:

Post a Comment