KIKOSI cha Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" ambacho leo Oktoba 7,2015 kimeilaza timu ya taifa ya Malawi "The Flames"bao 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
KIKOSI cha Taifa Stars ya Malawi "The Flames" ambacho leo Oktoba 7,2015 kimekubali kichapo cha bao 2-0 kutoka timu ya taifa
ya Tanzania "Taifa Stars" katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Baoooooooooooooooooo!!!
Shangwe za bao
Na Lenzi ya Michezo Blog
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo imetakata baada
ya kuifunga Malawi `The Flames’
kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia uliofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mabao ya Taifa Stars yalifungwa na wachezaji wa Tanzania
wanaocheza soka la kulipwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Mabao yote ya Taifa Stars yalifungwa katika kipindi cha
kwanza huku Samatta akiwa wa kwanza kuwainua wapenzi wa soka nchini kwa bao
lake katika dakika ya 18 akipokea pasi safi kutoka kwa Ulimwengu.
Ulimwengu alifunga la pili katika dakika ya 20, baada ya
kipa wa Malawi, Simplex Nthala kutema mkwaju wa krosi wa Haji Mwinyi na
Ulimwengu akauwahi mpira huo na kuusukumia kimiani na kuihakikishia Taifa Stars
ushindi.
Mechi ilikuwa ni ngumu kwa kila upande, Malawi ndiyo
waliopeleka mashambulizi mengi zaidi ya Taifa Stars hasa kataika dakika 15 za
mwanzo.
Lakini kuanzia dakika 20 hadi 35, Stars walionekana
kuutawala mpira zaidi lakini Malawi hawakuwa wamelala, kwani nao walifanya
mashambulizi ya kushtukiza.
Ushindi wa Taifa Stars ni faraja kubwa kwao, ambayo mara
mbili ilicheza na Malawi katika mechi za kimataifa za kirafiki, Mwanza na Mbeya
kwa nyakati tofauti na kutoka sare ya kufunga 1-1, na ile ya suluhu.
Pia ni furaha iliyoje kwa kocha wa Taifa Stars, Charles
Mkwasa ambaye juzi tu aliingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuwa kocha
mkuu wa timu hiyo baada ya awali kuwa na mkataba wa miezi mitatu kama kocha wa
muda.
Mkwasa alipewa mikoba ya kuifundisha Taifa Stars kwa muda
baada ya kutimuliwa kwa kocha Mholanzi Mart Nooij baada ya timu hiyo kufanya
vibaya katika michezo mingi ikiwemo ya kimashindano na kirafiki.
Mbali na Mkwasa, Hemed Morocco naye alilamba mkataba kama
msaidizi wa Mkwasa kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja na nusu.
Tangu Mkwasa aanze kuifundisha timu hiyo imeshapata sare
mbili dhidi ya Uganda katika mashindano ya Kombe la Chan ya mabao ya 1-1 na
dhidi ya Nigeria ya 0-0 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya
Afrika (Afcon).
Samatta amekuwa msaada mkubwa kwa TP Mazembe baada ya hivi karibuni kuiwezesha timu hiyo kutinga
fainali ya Ligi ya Mabigwa wa Afrika baada ya kufunga mabao mawili wakati
wakishinda 3-0.
TP Mazembe katika
mchezo wa awali ilifungwa mabao 2-1 na kuifanya kutinga fainali kwa ushindi wa
jumla ya mabao 4-2, ambapo sasa itacheza na USM Alger ya Algeria.
Fainali hiyo itapigwa
kati ya Oktoba 30 na Novemba mosi wakati ule wa marudiano utafanyika kati ya
Novemba 6 na 8.
No comments:
Post a Comment