October 29, 2015

RAIS KIKWETE AMPONGEZA DK MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
Rais Kikwete akimsomea Magufuli sms za pongezi kutoka kila pembe ya dunia.
Mkono wa Pongezi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete. 
Dk John Pombe Magufuli akipokea simu moja wapo za pongezi kutoka kwa Mgombea wa ACT Wazalendo, Anna Mgwira.
Mazungumzo na vicheko vya furaha vikiendelea

No comments:

Post a Comment