October 20, 2015

NDESAMBURO AMUOMBEA KURA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI JAFARY MICHAEL

Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake ,Philemoni Ndesamburo,akimnadi mgombea Ubunge katika jimbo hilo Jafary Michael (Chadema) katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata ya Ngangamfumuni.
Baadhi ya wananchi wakiwa kando ya barabara wakifuatilia mkutano huo.
Mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema,Jafary Michael akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chadema na mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Moshi mjini,Philemoni Ndesamburo (katikati) akiwa na mgombea udiwani kata ya Ngangamfumuni,Anthony (kulia ) na mgombea udiwani kata ya Longuo Raymond Mboya. (kushoto).
Mgo,bea Ubunge jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiomba kura .
Baadhi ya wafuasi na wananchi waliofika katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimumbea kura mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Ngangamfumuni,Anthony.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimuombea kura mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Rau,Peter Kimaro wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,kandaya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment