Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge wa jimbo la
Chalinze,Mh Ridhiwan Kikwete (kulia) pamoja na Mh.Shukuru
Kawambwa,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa wa shule
ya msingi majengo wilayani humo jioni ya leo.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John
Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi ya Bagamoyo mkoani Pwani
itasaidia kuimarisha uchumi na ujenzi wa viwanda nchini. Hayo ameyasema leo wilayani Bagamoyo katika mikutano yake
ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo
amesema gesi hiyo itasaidia ujenzi wa viwanda katika serikali take.
"Kwanza niwapongeze kwa kugundua gesi hapa Bagamoyo, tena
imegunduliwa katika eneo la ruvu. Na hii itakuwa na manufaa kwa uchumi
wa Taifa na kwa wananchi wa Pwani kwa ujumla.
"Gesi hii itasaidia sana ujenzi wa viwanda vya kisasa
katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano. Tutajenga viwanda na
tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi hii pamoja na Tanzania
yote," amesema Dk. Magufuli.
Umati wa wakazi wa mji wa Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi majengo wilayani Bagamoyo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa kampeni na kuomba kura za kutosha ili awe Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amemaliza kampeni zake ndani ya mkowa wa Kilimanjaro na leo ameanza mkoa wa Pwani,wilayani Bagamo ambapo anatarajia kuendelea na kampeni zake mkoani Lindi na mkoa wa Pwani.
Umati wa wakazi wa mji wa Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiwa wamekusanyika kwenye
uwanja wa shule ya Msingi majengo wilayani Bagamoyo wakimsikiliza
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa
akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa kampeni na kuomba kura za kutosha
ili awe Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Bagamoyo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa wa shule ya msingi majengo wilayani jioni ya leo.
Wananchi wa Hedalu wakiwa wamefunga barabara wakimzuia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli awasalimie na kumueleza shida zao ili akipata ridhaa ya kuwa Rais basi awasaidie kuyatatua matatizo hayo.
Wananch wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
Baadhi ya Wakazi wa Kiwangwa wakifuatilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipopita kuwasalimia akielekea wilayani Bagamoyo kwenye mkutano wa kampeni.PICHA NA MICHUZI JR-BAGAMOYO
No comments:
Post a Comment