Wasanii
nguli kutoka Tanzania wataungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika
msimu wa tatu wa maonyesho ya burudani ya muziki maarufu kwa jina la
Coke Studio Afrika ambalo litaanza Jumamosi wiki hii .Onyesho la mwaka
huu ni tofauti na yaliyopita kwa kuwa litaendana na mabadiliko yaliyopo katika
muziki duniani “Kolabo”na litarushwa na kituo cha televisheni cha Clouds
kuanzia saa 12 jioni.
Meneja wa Biashara za Coca-Cola nchini Maurice Njowoka
amesema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili
tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika
hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki
mchanganyiko lakini safari hii utatumika katika onyesho la Coke Studio na
utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa
wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema
Wasanii wanne kutoka Tanzania watakaokuwa kwenye
Kolabo la Coke Studio mwaka ambalo onyesho lake litaanza kuonekana kwenye
luninga Jumamosi ya Oktoba 10 ni Ben Pol ambaye atakuwa pamoja na mwanamuziki
nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi,Fid Q atakuwa pamoja na Maurice
Kirya kutokana Uganda,Gwiji wa Bongo fleva nchini Ali Kiba atashirikiana
na Victoria Kimani kutoka nchini Kenya na Vanessa Mdee atakuwa pamoja na
mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.
Maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa Coke Studio
Afrika yamekamilika na wapenzi wa muziki nchini wanasubiri kwa hamu kuwaona
wanamuziki wanaowashabikia wakiwasha moto kwa kushirikiana na wanamuziki
kutoka nje ya nchi na hii inadhihirisha kuwa onyesho la Coke Studio litaacha
historia ya pekee katika fani ya muziki nchini.
No comments:
Post a Comment