August 10, 2015

MBUNGE VITI MAALU CLARA MWATUKA WA CUF AFARIKI KATIKA AJALI

Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi CUF, Mh. Clara Mwatuka, amefariki dunia jioni ya leo kwa ajali baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuja Ndanda.

Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake,ambaye inasemekana ni mwanae.Maiti ipo Hospitali ya Rufaa ya Ndanda, Mkoani Mtwara.

Father Kidevu Blog inaungana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu, na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahala pema Peponi AMEN.

No comments:

Post a Comment