January 05, 2015

MISS SINGINDA 2014, DORIS MOLLEL AKABIDHI MSAADA HOSPITALI YA MKOA

Doris Mollel akisema Maneno machache wakati akikabidi mashine mbili za watoto kupumulia zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa  ushirikiano na Manifester brand.
*******
Na mwandishi wetu, Singida.
Katika kuianza safari yake ya huduma za jamii kwa mwaka 2015, Redds Miss central zone2014-2015 Doris Mollel ametoa msaada wa mashine 2 za kupumulia kwenye hospitali ya mkoawa Singida zenye thamani ya Tsh 1,200,000/=. Mashine hizo huwasaidia watoto waliozaliwakabla ya muda wa kawaida (Pre-mature babies) katika mfumo wao wa upumuaji ambao huhitajimsaada wa juu zaidi mara tu wanapozaliwa.

Doris ambaye pia ni mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2014 ni mwanaharakati wadhana ya Urembo wenye Malengo endelevu kwa jamii ‘Beauty with a Purpose’. Amefanyakazi kubwa kwenye sekta ya elimu akijikita zaidi kwenye kuchangia Vitabu kwa shule za msingina sasa, akiwa ni mmoja ya watu ambao walizaliwa kabla ya muda wa kawaida ameamuakupanua wigo wake wa huduma za jamii kuleta mwamko na kusaidia kuokoa maisha ya watotohawa.

Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo iliyofanyika hospitalini hapo, Mollel alisema.“Kiwango cha vifo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya kukomaa ni karibu 30% vikichangiwa kwakiasi kikubwa na ukosefu wa vifaa vya kutosha kusaidia mifumo yao ya upumuaji mara tuwanapozaliwa. Nikiwa moja ya watoto hao ambaye nilibahatika kupata msaada na huduma yakutosha nilipozaliwa, Ninaelewa ni jinsi gani matunzo haya ya awali yalivyo muhimu kwenyekuokoa maisha ya watoto hawa na ninajikita kuwasaidia”

Bw. Albert Mbepera, Mkurungezi wa Albert Manifester Photojournalism; kitengo ndani ya Manifester brand kilichojikita kwenye masuala ya jamii alisema ‘huduma kwa jamii ni eneo muhimu sana kwetu. Tunafurahi kujitolea kufanya kazi na Doris katika maswala ya kusaidia jamii na tunaamini kuwa ushirikiano huu utasaidia kukusanya na kuonyesha matatizo ya wahitaji ili kuongeza uelewa na msukumo wa misaada kutoka kwa sekta binafsi na wanajamii kwa ujumla’

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi Queen Mlozi na ilihudhuriwa na Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Bw. Daniel Tarimo, Daktari bingwa wa watoto wa Hospitali ya Singida, Muandaaji wa Redds Miss Singida 2014 Bora Lemmy na washindi wengine wa Redds Miss central Zone Linda Bureta, blath Chambia, Suzy Wahere.

Doris akikabidhi mashine 2 za msaada wa watoto kupumulia zenye thamani ya Tsh milioni 1.2 kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Daniel  Tarimo, msaada kwa ushirikiano na Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hii alikua ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi (hayupo pichani).
 
Doris katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi, Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Daniel Tarimo, Muandaaji wa Miss Singida Bi. Bora Lemmy na warembo wengine wa Redds miss Central Zone.

Doris kwenye picha ya pamoja na warembo wenzake wa central zone walioenda kumuunga mkono. Linda Bureta, Blath Chambia na Suzy Wahere.


 Doris akiangalia mmoja wa watoto
 Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wa kawaida akiwa kwenye mrija wa kumsadia kupumua uliounganishwa na mashine kama ambazo zimekabidhiwa na Doris.

 Alipata nafasi ya kuwasimulia baadhi ya kina mama waliojifungua watoto njiti kuhusu historia yake na kuwapa moyo kwamba hata watoto wao pia watakua na kufanikiwa kufika popote pamoja na kuzaliwa njiti.

No comments:

Post a Comment