George Masaju (kushoto) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika.
*******
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.
Uteuzi
wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa,
Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla
ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana
Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment