Timu
ya Tanzania jana wailiichapa timu ya EALA mabao 4 kwa 0 ambapo Mh.
Joshua Nassari alifunga bao la kwanza na bao la pili kufungwa na na
mchezaji mahiri Yusuph Gogo na la tatu kufungwa na Ahmed Ngwali na bao
la nne timu ya EALAwalijifunga wao wenyewe kupitia kwa beki wao Wyclif
Keto katika harakati za kuokoa mpira
Timu ya EALA
Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima kiongozi wa timu ya Tanzania akiwa
katika picha ya pamoja na waamuzi wa mechi kati ya Tanzania na EALA jana
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Mashabiki wakiwa wanafatilia mpambano kati ya Tanzania na Bunge la EALA jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Mlinda malango timu ya Tanzania Mh.Idd Azan akijiweka sawa golini kuhakikisha magoli hayaingii
Mlinda mlango timu ya EALA akiwa anajiandaa kudaka mpira
Dk Hamisi Kigangwala mchezaji wa Tanzania akiwa uwanjani
Mh.Joshua
Nassari mchezaji wa timu ya Tanzania akiwa amenyanyua fulana yake juu
mara baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza ujumbe ulikuwa ukisomeka
hivi"ESCROW hela zetu"
Muonekano wa wachezaji uwanjani
Mabalozi kutoka Model of Tourism Tanzania wakiwa wanashangilia wakati timu ya Tanzania na EALA wakipambana uwanjani
No comments:
Post a Comment