December 14, 2014

TANGAZO LA KIFO CHA MAMA MZAZI WA AKINA MWAIBALE

Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake

Familia ya  Mwaibale inatangaza kifo cha mama yao mpendwa, Twitikege Mlagha Mafumu kilichotekea leo saa 5 usiku wakati akipelekwa  Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa mtoto wake Mwalimu Mary Anyitike, eneo la Bucha Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam.

Kwa mawasiliano zaidi  wasiliana na ndugu Kulwa Mwaibale kwa simu namba 0712-707630, O758-971351 na Dotto Mwaibale kwa namba ya simu 0712-727062, O786-858550, 0754-362990.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment