Radio
5 FM 105.7 imeandaa "kampeni ya RADIO 5 viwanjani" katika mkoa wa
Arusha ambapo itawakutanisha watangazaji na madjs na wasikilizaji wao
katika kumbi za starehe kwa takribani wiki tano ikiwa ni sehemu ya
kuwashukuru mashabiki wa Redio hiyo kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima huku
mashabiki wakijipatia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo(katika picha ni
Mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Julius Kamafa aliyejizolea umaarufu
mkubwa jijini Arusha kupitia kipindi chake cha funiko base
kinachosikilizwa zaidi na vijana akishow love na msikilizaji wake katika
kampeni ya "Redio 5 viwanjani"ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda jijini Arusha
Timu kazi ya Redio 5 wakifatilia show
Mtangazaji
maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha love
cuts Semio Sonyo akiwa anauliza maswali kwa vijana wa Arusha waliofika
katika kampeni ya Redio 5 viwanjani ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda jijini
Arusha
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akifurahia jambo katika kampeni ya Redio 5 viwanjani iliyofanyika jijini Arusha
Mtangazaji
maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha love
cuts Semio Sonyo akimuuliza maswali shabiki wa redio 5 katika kampeni ya
Redio 5 viwanjani yenye nia ya kuwashukuru wasikilizaji wa kituo hicho
kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima
Meneja
ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto akieleza nia ya kampeni hiyo
itakayofanyika katika bar mbalimbali jijini hapa ambapo pia wasikilizaji
wa kituo hicho watajizolea zawadi mbalimbali zikiwemo
T-shart,vikombe,vinywaji kutoka TBL
Shabiki wa Redio 5 aka chali ya Arachuga akionyesha kiduku cha Arushaaaa. Picha zaidi
No comments:
Post a Comment