December 31, 2014

MTUHUMIWA ALIYEJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU APIGWA RISASI


Na Father Kidevu Blog
Mshitakiwa wa kesi ya kukutwa na dawa za kulevya Abdul Koroma (33) amekufa papo hapo baada ya kupigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam.

Koroma ambaye ni raia wa Sierra Leone, alifikishwa mahakamani hapo na kuomba kwenda kujisaidia, akiwa chooni alivua suluari yake ya jinsi na kuitumia kama ngao ya kujikinga na chupa zilizoungu ukuta wa choo cha mahakama, akafanikiwa kuruka na kuanza kukimbia.

Kwamujibu wa mashuhuda, askari magereza alimuona na kuanza kumkimbiza huku akifyatua risasi mbili hewani kumtahadharisha, lakini aliendelea kukimbia kwa lengo la kuruka uzio wa Mahakama.

Mlizi wa mahakama hiyo alijaribu kumzuia kwa kumshika miguu ili asiruke lakini wakati mapambano yanaendela askari alifyatua risasi iliyompat Koroma ubavuni karibu na kwapa na kupita hadi kichwani, akaanguka juu ya uzio wa mahakama hiyo.

Koroma alikuwa katika gereza la Keko, akikabiliwa na kesi namba PI 21 ya mwaka 2013 kwa madai ya kukutwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akisafirisha gramu 1229 za dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya Sh milioni 61,482,50.

Upande wa Mashitaka katika kesi hiyo wanasubiri hati ya kifo ili wafute mashitaka dhidi yake na  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katikaHospitali ya Taifa ya Muhimbili.

No comments:

Post a Comment