Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego anatarajiwa kulipamba Tamasha
la amani linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi hii desemba 20 katika
viwanja vya Sheik Amri Abeid lililoko mkoani Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mratibu wa Tamasha hilo Bertha Ismail kupitia
kampuni ya Bimo media alisema kuwa Msanii huyo anaetamba na wimbo wake
wa “Nakula Ujana” anatarajiwa kutua mkoani Arusha siku ya Alhamisi ya
desemba 18 na timu yake nzima ambapo atafanya matangazo katika sehemu
mbalimbali za jiji la Arusha kuhamasisha watu kuhudhuria tamasha hilo.
“Mbali
na wasanii wengine wa Arusha, Msanii mkubwa ambae anatarajiwa kulipamba
tamasha hilo ni Ney wa Mitego ambae tunaamini kwa Arusha atavuta watu
wengi kuhudhuria tamasha katika uwanja wa Sheik amri abeid kuja
kusikiliza ujumbe wa Amani ambapo utatolewa na Mgeni Rasmi”alisema
Bertha.
Alisema
kuwa Tamasha hilo litakalohudhuriwa na viongozi mbali wa serikali,
Tasisi pamoja vyama vya siasa, lengo kubwa ni kuwaunganisha vijana na
kupata ujumbe wa amani hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi
mkuu wa mwakani, ujumbe utakaotolewa na msajili wa vyama vya siasa
nchini Jaji Francis Mutungi.
“Tunapoelekea
uchaguzi tunajua mara nyingi sisi vijana ndio tunaotumika zaidi, hivyo
lengo kuu la Tamasha hili ni kuwaunganisha vijana katika umoja ili
wasigawanywe kwa misingi ya dini na siasa hali itakayojenga chuki na
kufanyiana fujo, hivyo wasifanye hivyo bali kila mmoja atumikie chama
chake au dini yake kwa amani bila vurugu”
Bertha
alisema kuwa Tamasha hilo lililodhaminiwa na kiwanda cha soda cha
pepsi, Kituo cha redio five na Sunrise Arusha, Mbali na Burudani ya Ney
wa mitego pia kutakuwa na burudani zingine kama Ngoma za asili,
sarakasi, maonyesho ya warembo wa mitindo pia vijana chipukizi wa Arusha
wataimba nyimbo mbali mbali sambamba na Watangazaji wa redio za Arusha
kukimbia riadha hivyo kutumia fursa hiyo kuwaalika wadhamini kutumia
nafasi hiyo kutangaza bidhaa zao kwa kushiriki tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment