December 30, 2014

MKESHA WA MWAKA MPYA NDANI YA SAFARI CARNIVAL

Na Andrew Chale
SAFARI Carnival kwa kushirikiana na Asia Idarous Khamsin (Fabak fashions) usiku wa 31/12/2014, Wameandaa shoo maalum ya Mkesha wa mwaka mpya 'Old Is Gold taarab', Ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Kawe jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin alieleza shoo hiyo maalum wadau mbalimbali watakutana kuupokea mwaka kwa pamoja huku wakipata burudani ya muziki wa taarab wa zamani 'Old is Gold' pamoja na 'Surprise' kibao.

"Kwa kiingilio cha sh 5,000, tu, Fabaki fashions na Safari Carnival, tumeandaa usiku huu maalum wa Mkesha wa mwaka mpya.

Utakaoambatana na burudani ya taarab za zamani na za sasa pamoja na Surprise mbalimbali" alisema Asia Idarous.

Aidha,  Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na Michuzi Media Group, Clouds fm,Gone Media, Maji Poa na wengineo.

No comments:

Post a Comment