December 03, 2014

MAZISHI YA MRAKIBU WA POLISI CAPT.KIDAI SENZALA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA HEKOPTA DAR ES SALAAM

Maafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014.

Marehemu Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya maziko yake. 

Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya kupata hitlafu katika injili yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba,  Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa Arusha.
Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
 Wanafamilia wakiwa katika gari lililobeba mwili wa mpendwa wao Capt. Kidai Senzala.
 Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
 Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.
 Heshima zikiendelea...

Ndugu wa marehemu akiwepo mkewe, mama yake mzazi marehemu, dada zake na ndugu wengine wakitafakari kazi ya Mungu baada ya kufanyika kwa mazishi ya Capt. Kidai Senzala.

No comments:

Post a Comment