December 16, 2014

MARCIO MAXIMO ATUPIWA VIRAGO YANGA NI BAADA YA KICHAPO CHA 2-0 KUTOKA SIMBA

YANGA SC imeirejea historia yake ya kuwatimia makocha wake muda mfupi tu baada ya kula kichapo kutoka kwa watani zao Simba ambapo tayari uongozi wa Yanga umelivunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa na makocha Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva na kuwarejesha Mholanzi, Hans Van der Pluijm na  Charles Boniface Mkwasa 'Master'.

Maximo anaondolewa baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, wakati Pluijm anawasili usiku huu na kesho atasaini Mkataba na kuanza kazi. Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.

Maximo na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni. Hata hivyo baada ya muda usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya kiufundi.
 
Pluijm alirudi Ghana wakati Mkwasa alirejea nyumbani Tanzania kabla ya kuajiriwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Mkufunzi Mkuu.

1 comment: