December 12, 2014

DK PINDI CHANA (MB) KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, MKOANI NJOMBE

 Dkt. Pindi Chana akiwanadi wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Mtaa wa Kihesya na Kwivaha, Njombe Mjini.
Mheshimiwa Dkt Pindi Chana(Mb.), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Tarehe 10/12/2014 alifanya ziara ya kikazi ya chama Mkoani Njombe kwa kushiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katika ziara hiyo pamoja na shughuli nyingine Mhe. Mbunge aliwanadi wagombea uongozi kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Mtaa wa Kwihava na Kihesya, Njombe Mjini.

Kupitia mikutano hiyo ya kampeni wagombea walipata fursa ya kueleza sera na ahadi zao kwa wananchi, endapo watawapa ridhaa ya kuwaongoza.

No comments:

Post a Comment