September 04, 2014

FALCAO: NILIANZA MAZUNGUMZO NA MANCHESTER UNITED MIEZI 4 ILIYOPITA

Radamel Falcao (wapili kushoto) akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Colombia huko Miami. 

Mshambuliaji Nyota aliyesajili na Manchester United, Radamel Falcao amebainisha yakuwa alikuwa katika mazungumzo na mashetani hao wekundu takriban miezi minne iliyopita.

Nyota huyo kutoka Colombia amesema alikuwa tu akificha ukweli kwa mabosi zake wa zamani wa Real Madrid kabla ya kuhamia kwakwe Old Trafor.

Falcao alibainisha hayo wakati akihojiwa juu ya maandalizi dhidi mchezo wa kirafiki baina ya timu yake ya Colombia na Brazili utakao pigwa kesho amesema" Ninajisikia furaha sana kuichezea Manchesta United"

No comments:

Post a Comment