January 15, 2014

TBS YAENDESHA MSAKO WA BIDHAA ZISIZO NA UBORA

 Askari Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam wakibeba maborota ya mitumba ya nguo za ndani kama sidiria na chupi leo katika soko la Karume katika operesheni ya kukataza kuuza nguo za ndani za mitumba ambapo operesheni hiyo ikiendeshwa na shirika la Viwango Tanzania (TBS)
 Marobota ya nguo za ndani yakipakizwa katika magari ya polisi leo wakati shirika la viwango Tanzania Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini wakati walipoendesha operesheni Kataza kuuza nguo za ndani ambazo zishatumika(mitumba)
 Askari Polisi wakiendelea na operesheni hiyo katika Soko la Karume huku wafanyabiashara wa Sokoni hapo wakishuhudia zoezi hilo
 Magari ya polisi yakiwa Yamebeba Marobota ya Mitumba ya Nguo za Ndani mapema leo katika Soko la Karume katika Operesheni kataza kuuza nguo za ndani za mitumba
 Msafara kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi kwaajili ya kupeleka Mzigo uliokamatwa wa nguo za ndani zilizotumika almaarufu kama mitumba kwaajili ya kuteketezwa na moto wakati wa operesheni kataza kuuza mitumba ya nguo za ndani
 Msafara wa polisi ukielekea Kituo Cha Msimbazi mapema leo mara baada ya Kukamata wafanyabiashara na bidhaa zao za nguo za ndani za mitumba
 Msafara ukiingia Katika kituo cha Msimbazi 
 Mzigo Ukiwasilishwa katika kituo cha Polisi Cha Msimbazi Kwaajili ya kwenda kuteketezwa na Moto
 Mmoja wa Wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akishusha sidiria za mitumba ambazo zimekamatwa leo katika operesheni kata kuuza nguo za ndani za mitumba
 Mzigo Ukishushwa mara baada ya kufikishwa katika Kituo Cha Polisi Cha Msimbazi
Afisa Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukamata marobota ya nguo za ndani ambazo zimeshatumika wakati Nguo hizo zilishapigwa marufuku kuuzwa nchini.Picha zote na  Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment