Waziri Wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akimkaribisha Naibu wake Juma Nkamia ofisini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fennela Mukangara
akimkaribisha Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia katika Ofisi za Wizara zilizopo katika jengo la
Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma
Nkamia akiongea na Wanahabari Ofisini kwake katika tukio la
kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.Picha na Benjamin Sawe.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la
kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bwana Clement Mshana (kushoto)
akimpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia wakati wa mapokezi yake
katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam leo katikati ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Elisante Olegabriel.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma
Nkamia akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bwana Kulwa
Magingila wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.
No comments:
Post a Comment