Wakati ikiwa imesalia miezi 22 kabla ya kufanyika kwa ucvhaguzi mkuu wa Serikali mwaka 2015, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama kuziba nafasi zilizo achwa wazi huku wengine wakibadilishwa maeneo yao ya kazi.
Akitangaza mabadiliko hayo leo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Kikwete amewatupa nje viongozi kadhaa akiweomo Waziri wa Mazingira, Dk. Theresia Huvisa pamoja na Manaibu waziri, Goodluck Ole Medeye aliyekuwa Ardhi, Philipo Mulugo- Elimu, Benedict Ole Nangoro- Naibu Mifugo na Uvuvi.
Akiulizwa swali na wanahabari juu ya kuendelea kuwapo kwa mawaziri 'Mizigo' ambao walilalamikiwa na Bunge na hata vyama vya siasa, Balozi Sefue alidai kuwa hilo linatokana na namna gani Wizara iliwezeshwa katika kutekeleza majukumu yake.
Mabadiliko na uteuzi huo kamili ni kama ifuatavyo:-
OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko
Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).
Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri
OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
WIZARA:
WIZARA YA FEDHA
Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) – Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) – Naibu Waziri wa Fedha
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)- Naibu Waziri wa Fedha
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)-Waziri wa Katiba na Sheria
Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) – Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)- Waziri wa Mambo ya Ndani
Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)- Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)- Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) – Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)- Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) – Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
WIZARA YA MAJI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)- Naibu Waziri wa Maji
WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) – Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) – Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)-Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko
Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)
Balozi Ombeni Y. Sefue (Pichani juu).
KATIBU MKUU KIONGOZI
Ikulu
DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014
No comments:
Post a Comment