Meneja
wa bia ya Castle Lite, Victoria Kimaro kulia akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam juu ya kufanyika kwa Tamasha kubwa la musiki kwenye jiji
la Johannesburg nchini Afrika kusini ambapo jumla ya watanzania 12 watashinda
tiketi za kushudia tamasha hilo litakaloongozwa na mwanamusiki nguli duniani
TIMBALAND, Kushoto ni meneja mawasiliano
na habari wa TBL Edith Mushi.
********
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Castle Lite
imezindua promosheni maalum, ili kupata watu 12 ambao watakwenda Afrika Kusini
kushuhudia onyesho kubwa la msanii maarufu duniani, Timbaland.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Habari
na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi alisema, promosheni hiyo itaendeshwa kwa
miezi mitatu kuanzia Januari 20 hadi Machi 30, mwaka huu.
Edith alisema, droo ya mwisho inatarajiwa kufanyika Aprili 7 na washindi
hao watakwenda katika tamasha hilo kubwa la muziki linalotarajiwa kufanyika Johannesburg,
Aprili 26, mwaka huu.
“Kutakuwa na zawadi mbalimbali za kuvutia zitakazotolewa kwa washindi,
lakini zawadi kubwa kuliko zote ni ile safari ya kwenda Afrika Kusini
kushuhudia tamasha hilo kubwa la muziki.
“Washindi hao 12 watalipiwa gharama zote za usafiri, malazi, chakula na
usafiri wa ndani wakiwa Afrika Kusini na mambo yote haya yatafanywa katika
kiwango cha hali ya juu, watahudumiwa kama waheshimiwa,” alisema.
Naye Meneja wa Castle Lite, Victoria Kimaro alisema, mteja anatakiwa kununua
bia hiyo ya chupa akifungua ataona namba zilizowekwa ndani ya kizibo, atatakiwa
kutuma jina lake na namba hiyo kupitia ujumbe mfupi wa simu kwenda kwenye namba
15499.
‘Nawasihi wapenzi wa Castle Lite, kujitokeza kwa wingi kushiriki promosheni
hii ya aina yake na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali zilizoandaliwa kwa
ajili yao hasa zawadi hiyo kubwa ya kwenda kumshuhudia Timbaland.”
Pia aliwaomba wapenzi wa Castle Lite kutembelea ukurasa wa Face Book wa
Castle Lite ili kuweza kupata maelezo zaidi ya promosheni hii, ikiwemo vigezo
na masharti.
Castle Lite ni kinywaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment