Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amejiuzulu wadhifa
wake baada ya mjadala mkali na wakina Bungeni mjini Dodoma leo jioni.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini.
Tangu
kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka
kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa
wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo
kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni
hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (Tanapa).
Operesheni
hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao
kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. John Nchimbi, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo
wawajibike.
Waziri Kagasheki atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya siku za hivi karibuni katika kamata kamata ya pembe za ndovu.
No comments:
Post a Comment