Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoaniLindi, ambaye pia ni Kamishna msaidizi wa Jeshi hilo,Acp Renatha Mzinga,akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Muuguziwa kambi ya wazee wasiojiweza wa Rasibura,Manispaa ya Lindi,Bi,Elizabeth Njowele
********
MTANDAO Wa Polisi Wanawake Mkoani Lindi (TPF-net) Umeipatia kambi ya wazee wasiojiweza msaada wa bidhaa mbalimbali,zikiwemo nguo, vyakula na mafuta wenye thamani ya Sh,309,500/-ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya mwanamke hapa nchini.
Bidhaa hizo ni,mchele,unga,Sukari, nyama ya Ng’ombe ,mafuta ya kupakaa na kupikia,Sabuni za kufulia na kuogea,dawa za meno na miswaki,ndoo mbili aina ya Plastic kwa ajili ya kuhifadhia maji,leki za kuzolea taka na Brashi za kusafishia vyooni.
Akikabidhi msaada huo,mwenyekiti wa Mtandao huo na Ambae pia ni kamishna msaidizi Polisi mkoani Lindi Acp Renatha Mzinga,alisema wao wakiwa ni wanawake wa jeshi hilo,wameamua kuchanga kidogo walichonacho kutoka sehemu ya posho zao,ili kuwakumbuka wenzao wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo wazee na walemavu wasiojiweza ikiwa katika kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya mwanamke, yaliyoanza Novemba 25 na kukamilika Decemba 10 Acp Mzinga amesema iwapo wazee hao wangekuwa na viungo vyao kamili pamoja na kuwa na maisha mazuri,wasingependa kubaki kuishi katika kambi hiyo,huku wakisubiri kusaidiwa kutoka kwa watu wengine.
“Kama msingekuwa na ulemavu kama mlivyokuwa hivi sasa,msingekuwa na sababu za kuishi katika mazingira ya aina hii hivyo sisi tumeona ni bora tuje tuwafanyie Usafi wa makazi yenu na tuwapatie msaada mdogo uliotokana na michango yetu..alisikika kamanda Mzinga wakati akikabidhi misaada hiyo.
“Yapo maneno yanazungumzwa na baadhi ya watu kuwa kutoa ni moyo na sio utajiri,wangapi wana mali nyingi tu, lakini hata siku moja hatujaweza kuwaona wakifika hapa kutufariji kwa kile walicho nacho,,,,,,,,,,,,Hivyo hiki mlichokitoa ingawaje mnakiona ni kidogo lakini kwetu sisi tunakiona ni kingi na mbele ya mungu anaiona dhamira yenu kuwa mmeonesha nia ya kutusaidia wenzenu”Alisema Chitawala.
Chitawala alisema kitendo cha Mtandao huo kuwasaidia wazee wa kambi hiyo, sio ni furaha bali ni moja ya sehemu utekelezaji wa maagizo ya mwenyezimugu wetu kupitia kwenye vitabu vyake anavyoutaka viumbe vyake walio na uwezo kuwasaidia wenzao wasio na na uwezo wakiwemo wao
walemavu.
Katika kambi hiyo,iliyo chini ya kanisa katoriki Jimbo la Lindi,imebaki na wazee walemavu wasiopungua saba (7) wakiwemo wanawake watano na wanaume wawili,kati ya 15 waliokuwepo hapo awali,kufuatia baadhi yao kufariki dunia na wengine kuamua kuondoka kambini hapo,kutokana na kile kinachodaiwa huduma duni wanazozipata katika kambi hiyo.
No comments:
Post a Comment