December 15, 2013

Rais Kikwete ampa pole Lowassa

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole na kumrekebisha tai mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambaye juzi alinusurika katika ajali ya ndege baada ya ndege aliyokuwa akisafiria  inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Precision kupasuka matairi yote ya nyuma wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa mjini Arusha. Rais Kikwete alikuwa Monduli Mkoani Arusha kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania katika chuo cha jeshi Monduli.

No comments:

Post a Comment