December 17, 2013

NSSF YABEBA TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI 2013

Meneja wa NSSF mkoani Tanga, Frank Maduga
MSIMU wa kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni, lililokuwa  likisubiriwa kwa hamu hatimaye lilifanyika Juzi, wilayani Handeni  Tanga  ambapo kama ilivyokuwa ikitarajiwa, Shirika la Taifa la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilijitokeza na kubeba tamasha hilo.
Shirika hilo, likiwa limejitokeza dakika za mwisho katoa udhamini wake katika tamasha hilo kubwa na la kwanza kuwahi kufanyika katika Ardhi  ya wilaya ya Handeni linalojumuisha vijiji zaidi ya kumi, lilichangia fedha taslimu shilingi milioni mbili, fedha ambazo kwa kiasi kikubwa ukiacha mchango wa wahisani wengine zilichangia  kufanikiwa kwa Tamasha hilo.

Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema kukiwa na dalili zote za tamasha kushindwa kufanyika kama ilivyotarajiwa, NSSF kupitia Ofisi ya kanda ya Tanga ilijitolea kunusuru Jahazi.
Mratibu wa Tanmasha la Utamaduni Handeni-Kambi Mbwana akitambulisha Wadhamini wa Tamasha hilo lililofanyika Juzi katika uwanja wa Azimio, wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akimkaribisha mmoja wa wahisani wa Tamasha
Mkurugenzi wa Grace Products akitoa neno la Shukrani kwa Waandaji wa Tamasha


“Awali ya yote napenda kutanguliza shukurani zangu zote kwa wahisani wa Tamasha hili, Vodacom, Grace products pamoja a wadhamini wengine kwa kufanikisha Tamasha hili la kwanza kuwahi kuwakutanisha watu wa kadhia mbalimbali,
JKT walikuwepo wakafanya yao jukwaani ilikuwa ni noma saaaana
Utamu wa Ngoma uingie uicheze
DC Muhingo Rweyemamu

Shukurani kubwa ziende kwa NSSF, kwa kweli hawa watu wanajali utu, tunaomba watusamehe kwa mapungufu yetu lakini kwa kweli wanastahili kuitwa mfuko wa Hifadhi,” alisema Kambi
Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.
Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa eneo Fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti kama waratibu wa Tamasha hilo walivyofanya.
Vyakula vya Asili hapa palikuwa ni mahala pakee

“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, Hongereni sana,” alisema Rweyemamu.
Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa Tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa.
Mamia ya Waandamanaji wakielekea katika Viwanja vya Azimio
Taem Tamasha la Utamaduni Handeni....chezea
Msanii kutoka katika kundi la Okalandima, akionesha uwezo wa kutafuna Moto, hii ni moja ya Vyakula vyetu huku Handeni hasa Kwamsisi, karibu Handeni Kwetu.....

Katika tamasha hilo,kulikuwa na vionjo mbalimbali vya Utamaduni wa Wanahandeni, ikiwa ni Pamoja na Ngoma za asili kutoka katika Vijiji vya wilaya ya Handeni kama vile, Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni Mjini.

Burudani kali na ya kuvutia iliyoonesha asili kamili ya Mtanzania ilitoka kwa Kundi la Sanaa la Jeshi la JKT Mgambo, Azimio Jazz band bila kusahau msanii wa kundi la Fataki, Machenja ambaye alipiga onesho
la kukata kiu akiwa na wana okalandima.

Tamasha la Utamaduni Handeni ambalo linafanyika kwa mara ya Kwanza lilidhaminiwa na NSSF, Clouds fm, Vodacom, Plan B, gazeti la Mwananchi, MICHUZI Blog, Kajunason Blog, Chichi Local Wear, Katomu Solar specialist, Dullah Tiles and Construction, Anesa Company Limited, Country Business directory, Jiachie Blog na TAIFA LETU.com.

No comments:

Post a Comment