Hata wakati yupo kifungoni katika
chumba chake kidogo cha gereza katika kisiwa cha Robben, Nelson Mandela alifanya
mazoezi kujiweka fiti kiafya na mwili na akili.
Enzi za ujana wake alipata kuwa bondia
wa uzani wa juu (Heavyweight), kama ambavyo anaonekana katika picha kadhaa
akijifua.
Mandela pia alikuwa akijifua na swahiba
wake na bondia wa uzito wa kati Jerry Moloi ambaye yeye ngumi kwake ilikuwa ni
kazi na sehemu ya maisha yake kwani rekodi yake inaonyesha kushinda mabambano
13, kupoteza 15 na kutoka sare 30.
Picha hii wakiwa juu ya jengo mjini Johannesburg.
Sanamu hii ya Nelson Mandela iliyotokana na picha hiyo hapo juu ikiwa imewekwa mtaani kumuenzi Bondia huyo mpigania uhuru wa Afrika Kusiani.
Katika kitabu chake mzee Nelson Mandela
alicho anza kukiandika akiwa gerezani cha, Safari ndefu ya Uhuru (Long Walk to
Freedom), Mandela anaelezea upendo wake katika mchezo wa ngumi wa ndondi (na
kwa nini alifanya hivyo):
“Mimi sikuwa na furahia mapambano
uliongoni katika ngumi sana kama sayansi ya yake inavyosema. Mimi
nilikuwa navutiwa na jinsi mtu anavyouongoza mwili kujikinga, na vile mwingine
akitumia mkakati wa kushambulia na kurui nyuma ili kupata ushindi katika mchezo”,
aliandika Mandela.
Ngumi ni usawa katika ulingo, lakini cheo,
umri, rangi, na mali ni vitu visivyo na maana. . . Mimi kamwe sijafanya
mapigano yoyote halisi baada ya mimi kuingia katika siasa.
Madhumini yangu makubwa yalikuwa katika
mafunzo; mazoezi ya ngumi yalinifanya kupiteza msongo wa mawazo. Baada
ya ya mazoezi ya jioni nilijihisi kiakili na kimwili ni mwepesi.
Nelson Mandela akirusha ngumi kwa Bigwa wa Masubwi wa zamani Duniani Mohamed Ally.
Nelson Mandela akiweka paling na Mkali wa ngumi duniani Lennox Lewis.
Nelson Mandela akiwa na Mkali wa ngumi duniani Mike Tyson.
No comments:
Post a Comment