Ndege
ya abiria aina ya Boeing 767 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian
Airlines) ikiwa imesimama nje ya Uwanja wa Ndege wa Arusha baada ya
kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwenye
uwanja huo kwa dharula.
Ndege
hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 200 na wafanyakazi 9. kabla ya kupaa
tena ilibidi abiria wote wateremke, na kupunguzwa mafuta ili kupunguza
uzito wa ndege hiyo. Abiria waliamuriwa kwenda kupandia ndege hiyo
kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
Tairi za ndege hiyo zikiwa zimejikita kwenye Udongo.
Hakuna anaeamini kama ndege hiyo imeweza kushuka uwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment