Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,
Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.
No comments:
Post a Comment