Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.
Taarifa kutoka wilayani Korogwe ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo zinasema kuwa watu 12 hadi sasa wamepoteza maisha kufuatia ajali ya basi la Shukrani.
Basi hilo lililotokea jijini Dar es Salaam kwenda Tanga lilipata ajali eneo la Kabuku kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni na kujeruhi watu wengine 93 kati yao watu 9 wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali za KCMC Mjini Moshi na MOI jijini Dar esa Salaam.
Father Kidevu Blog itawajuza zaidi juu ya ajali hiyo.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Korogwe wakitoa huduma kwa majeruhi.
DC wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akiwa Hospitalini hapo kutoa Huduma kwa Majeruhi.
Wananchi wa Korogwe wakiwa nje ya Hospitali hiyo ya Wilaya ya Korogwe.
No comments:
Post a Comment