November 08, 2013

WASHIRIKI 20 WA TOP MODEL 2013 WAINGIA KAMBINI JB BELMONT HOTEL

 Jumla ya washiriki 20 wanaowania taji la Top Model 2013 wameingia kambini jana katika Hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam kujiandaa na shindano hilo. Kwa mujibu wa waandaaji wa shindano hilo warembo hao watakuwa wakihama hama hotel ili kuwaweka vyema kisaikolojia. Mchujo wa wanamitindo hao ulifanyika katika mikoa mbalimbali nchini na kuwapata warembo hao.

Shindano hilo linaandaliwa na Kampuni ya Tanzania Top Model chini ya Mwenyekiti wake Jackson Kalikumtima na fainali zake zinataraji kufanyika mwezi desemba mwaka huu.
Washiriki wanaowania taji Tanzania Top model wakiwasili jana katikaHotel ya JB Belmon.

No comments:

Post a Comment