Meneja wa Smile Tanzania na Uganda Fiona McGloin (katikati) akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari jijini Arusha leo. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mtandao, Madaha
Francis na Mkuu wa Mauzo, Deo Ndejembi.
Leo, Smile Communications
Tanzania (Smile) inazindua huduma zake za Fourth Generation Long Term Evolution
(4G LTE) mkoani Arusha, ikileta mapinduzi ya intaneti yenye kasi kwa wafanyabiashara,
mashirika na wakazi wa ndani na wanaozunguka jiji la Arusha.
Smile inatoa intaneti yenye kasi zaidi
katika soko; mtandao wake 4G LTE hutoa huduma za intaneti kwa kasi ambayo watoa
huduma wengine hawawezi kuifikia. Mtandao wa Smile hutumia teknolojia ya
mawasiliano iliyoendelea zaidi na viwango vya ubora vinavyoendana na sehemu
nyingine duniani, na hutoa kasi isiyo na mpinzani, uhakika, ubora na urahisi wa
matumizi ambao huboresha matumizi ya mtandao.
LTE (Long Term Evolution) ambayo pia
inajulikana kama 4G LTE inawezesha upatikanaji wa intaneti yenye kasi zaidi kwa
sababu ndiyo kiwango cha teknolojia cha kisasa cha kizazi cha nne (fourth generation
– 4G) na inawakilisha mabadiliko ya hatua katika mageuzi kutoka kwenye
teknolojia zilizopo za mawasiliano bila waya (wireless) kama vile GSM-
2G/GPRS/EDGE na UMTS-3G/3.75G. 4G LTE ni kizazi kipya cha mtandao pamoja na
mawasiliano ya sauti na intaneti, na muundo wake unaoweza kubadilika na
kuboreshwa mara kwa mara, una hakikisha kuwa 4G LTE itabaki kuwa kiwango bora
zaidi cha huduma za intaneti na sauti kwa miaka ijayo.
"Smile ilizinduliwa jijini Dar es
Salaam tarehe 16 Mei 2013, na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani
Afrika kupata mapinduzi haya ya kiteknolojia. Tuna furaha kubwa kuwaletea
huduma hii jijini Arusha. Kama kitovu mashuhuri kimataifa ambacho kina sekta iliyo
kubwa, inayokua kwa kasi na yenye nguvu zaidi katika huduma za utalii na
taasisi mbalimbali za elimu, Arusha ina biashara nyingi, mashirika na watu
ambao watafaidika kutokana na huduma zenye intaneti yenye kasi, "alisema
Fiona McGloin , Meneja wa Smile Tanzania na Uganda.
"Smile tuna uhakika kuwa kutoa
intaneti ya kuaminika na yenye kasi zaidi, itachangia kwa kiasi kikubwa katika
maendeleo ya biashara zilizopo Arusha na pia kuwapa wakazi wa Arusha huduma
yenye kasi, ya kuaminika na gharama nafuu,” alisema Bi McGloin.
Katika sekta inayokuwa kwa kasi ya
mawasiliano hapa Tanzania, intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndiyo inaongoza kwa kuwa
na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara nne zaidi kuliko 3.75G. Smile inatoa wastani wa
kasi ya kupakua ya 6Mbps na kiwango cha 3Mbps kasi ya kupakia. Kwa teknolojia
hii, watumiaji wana uhakika wa kasi ya upakuaji na muhimu zaidi, kasi ya
upakiaji wa mafaili, barua pepe, taarifa, nyimbo na michezo; matumizi ya nyenzo
mbalimbali za kwenye mtandao, na kwa kuangalia video/TV bila kugomagoma.
"Tunajivunia kuwaletea intaneti
yenye kasi zaidi jijini Arusha ambayo inalingana na kasi na ubora wa intaneti
barani Ulaya. Smile sio tu kwamba tutatoa huduma ya intaneti peke yake, bali
tutatoa huduma ya intaneti yenye kasi zaidi, ya kuaminika na kwa bei ya
kiushindani na pia tuna nia ya kutoa huduma kwa wateja zenye kuridhisha,”
aliongeza Bi. McGloin.
Kama sehemu ya mpango wa kuwajibika
kijamii wa kampuni ya Smile, kampuni inatoa huduma za bure za intaneti yenye
kasi katika shule za kiserikali: hadi sasa, Smile imewezesha shule 10 jijini
Dar es Salaam na inaleta mpango huo katika jiji la Arusha.
Wateja wa Arusha sasa
wanaweza kujiunga na Smile kwa kutembelea maduka yetu ya rejareja ambayo
yanazidi kuongezeka ,duka la Smile mtaa wa
India, jiji la Arusha , au kwenye kioski ndani ya duka la E-Tronic,
gorofa ya kwanza, Njiro Complex, Arusha, au wasiliana na Huduma kwa Wateja kwa
barua pepe (customercare@smile.co.tz) au simu +255 (0)
222 199 840.
Kupata taarifa zaidi
kuhusu Smile tembelea tovuti: www.smile.co.tz.
No comments:
Post a Comment