Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikata mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wanafunzi waongeze bidii kwenye masomo kwani elimu haina mwisho.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwakaleli baada ya kumaliza kushiriki shughuli za kimaendeleo ya ujenzi wa madarasa ,maabara na nyumbza za walimu.
Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akiwasalimu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wajitahidikusona na kuepukana na vitendo vitakavyo waharibia maisha yao.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Mbunge wa Viti maalum wanawake mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa.
Mzee Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Katende ambapo alihimiza sana kuwa makini na vyama vinavyojita vya siasa kwani sasa vimeanza kupoteza muelekeo.
Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa Katende.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katende na kuwaahidi CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kusema ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa lazima tuhoji serikali pesa za maendeleo kwa nini haziji kwa wakati.
No comments:
Post a Comment